Home LOCAL JUMUIYA YA WAZAZI ILALA YAKABIDHI VIFAA VYA SHULE 

JUMUIYA YA WAZAZI ILALA YAKABIDHI VIFAA VYA SHULE 

Na Heri Shaaban (Ilala)

Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala imekabidhi daftari za shule box tatu shule ya Msingi Buguruni Moto Kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu .

Msaada huo ulikabidhiwa shule hapo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wa
Kata ya Ilala Sabry Abdalah ,baada kupokea mwaliko kutoka kwa Diwani wa Buguruni Busoro Pazi .

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Wazazi Sabry Abdalah, alisema Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala inaunga mkono Juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuunga mkono sekta ya elimu sera wa elimu bila malipo.

“Ziara hii ya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala shule ya Msingi Buguruni Moto tunashirikiana na Mlezi wa Jumuiya ya wazazi Imran Jaffar ,Jumuiya yetu Ina jukumu la kusimamia elimu ,Malezi na Mazingira “ alisema Sabry .

Mwenyekiti Sabry alisema wameonyesha ushirikiano kwa Diwani wa Buguruni Busoro Pazi katika Maswala ya elimu ugawaji wa box tatu za madaftari Wanafunzi waweze kusoma kwa bidii kukuza taaluma .

Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Ilala IMRAN JAFFAR alisema wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani Pamoja na kusimamia sekta ya elimu nchini

Mwisho

Previous articleDC JOKATE AZURU AFRIKA YA KUSINI KUTANGAZA ZAO LA MKONGE NA BIDHAA ZAKE
Next articleWANAHABARI MKOANI MOROGORO WAPAZA SAUTI MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here