Home LOCAL WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA SGR MWANZA-ISAKA CHENYE UREFU WA KM 341

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA SGR MWANZA-ISAKA CHENYE UREFU WA KM 341

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo 26 Machi 2023 amekagua Mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa SGR Mwanza-Isaka, Kipande cha Tano cha Ujenzi wa reli awamu ya kwanza Dar es Salaam Mwanza.

Kipande hiki cha Mwanza-Isaka kina jumla ya kilometa 341, hadi kukamilika kwake kitagharimu shilingi Trilioni 3.062.

Kipande hicho kitakuwa na jumla ya vituo vya abiria 10 na vituo viwili vya mizigo vya Fela na Isaka.

Maendeleo ya ujenzi huo umefikia asilimia 28.03 na ujenzi wa tuta ni asilimia 58.4 sawa na kilometa 136 kati ya kilometa 249 za njia kuu.

Mradi huo umetoa ajira zaidi ya 6,720 na kandarasi ndogo zenye thamani ya shilingi bilioni 80 hadi sasa.

Baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo huku akitoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa vifaa na mitambo inayotumika katika ujenzi huo.

Previous articleWAZIRI MKUU AZINDUA JENGO LA EMD MASWA
Next articleWAZIRI MKUU AAGIZA STENDI KUU BARIADI ITUMIKE KWA MABASI MAKUBWA NA MADOGO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here