Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kikao kazi kati ya WCF na Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika leo Machi 20, 2023 Bagamoyo mkonani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (kulia) akifafanua jambo alikuwa akifungua Kikao kazi hicho kilichofanyika bagamoyo Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (katikati) akifungua Kikao kazi kati ya Mfuko huo na Jukwaa la Wahariri Mjini Bagamoyo leo machi 20,2023 Bagamoyo. (kulia) ni, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile, na (kushoto) ni, Mkurugenzi wa Tathimini wa WCF Dkt. Abdulssalaam Omar.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile (kulia) akizungumza alipokuwa akitoa salamu za Jukwaa hilo katika Mkutano huo. (kushoto), ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge akizungumza allipokuwa akiwakaribisha Maofisa wa Taasisi hiyo kuwasilisha Mada mbalimbali kwenye kikao hicho.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bi. Anitha Mendoza akifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Mduma (hayumo pichani) katika kikao huo.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, BAGAMOYO.
MKURUGENZI wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, ametaja mambo makubwa manne ya kimaendeleo ambayo yamefanyika kwenye taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Mduma ameyasema hayo katika Kikao kazi kati ya Mfuko huo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika leo Machi 20,2023 Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo amesema kuwa kuna mambo makubwa manne ambayo yamefanyika katika kuboresha huduma za mfuko kwenye kipindi hiki cha Rais Samia.
Amesema mambo makubwa ambayo serikali ya awamu ya sita imeyafanya kwenye miaka yake hiyo miwili ni kuhakikisha mfuko huo unakuwa sehemu ya mafanikio katika kuifanya Tanzania inakuwa ni mahala pazuri pa kuwekeza na kufanya biashara.
“Miaka ya nyuma wafanya biashara walipaswa kuchangia asilimia 1 ya mshahara wa wafanyakazi wake, ilipoingia serikali ya awamu ya sita ilipunguzwa hadi asilimia 0.6 na mwaka huu wa fedha imeshushwa hadi asilimia 0.5 kiwango kinachochangiwa na Serikali kimelinganishwa na kile kinachochangiwa na sekta binafsi” amesema Dkt. Mduma.
Aidha, Dkt Mduma amesema serikali ya awamu ya Rais samia pia imepunguza riba kwa wanaochelewesha michango ambapo awali ilikuwa ukichelewesha unakutana na riba ya asilimia 10 kwa mwezi na kwamba mzigo huo ulikuwa mkubwa na kuwatishia waajiri ambao hawajajisajili, ambapo sasa serikali imeshusha hadi asilimia 2.
“Serikali pia imefuta madeni kwa ambao hawakuwa wamelipa kwenye kipande cha riba ambacho ilikuwa ni asilimia 10 kwa waliochelewesha, lakini pia madeni yao yalifutwa hivyo waajiri wa sekta binafsi walibaki kulipa deni la msingi. Hayo ni mambo makubwa ambayo yamefanyika kwenye kipindi hiki,” alisema
Aidha amesema kuwa maendeleo mengine ni ya ndani ya WCF ambayo ni matumizi ya Digitali, ambapo kwasasa kuna asilimia zaidi ya 85 ya huduma zao zinazo patikana (online) mtandaoni.
“Lingine linagusa mwananchi wakawaida taratibu zao za mafao zilitegemea kikotoo cha mshahara wa aliepata ugonjwa ama ajali na asilimia ya ulemavu aliuoupata hiyo ilichangia kama mtu alikuwa na mshahara wakima cha chini bado anazidi kurudi chini.
“Serikali imeweka kima cha chini cha fao kinachoweza kuwa kikubwa kuliko mshara wa huyo mtu aliyepata hayo majanga sio chini ya laki sita,” alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameupongeza uongozi wa WCF kwa kuongeza wigo wa kuwafikia wanufaika kwa wakati.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuushukuru Mfuko huo kwa kuonesha nia ya kushirikiana na TEF katika Mkutano wao Mkuu wa 12 wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Machi 29 hadi 31, 2023 Mkoani Morogoro.
Mwisho.