NA: TIMA SULTAN
KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kushinda mabao 7-0 dhidi ua Hoyora FC ya Guinea.
Simba imepata ushindi huo katika mchezo wake wa hatua ya makundi uliochezwa katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo Machi 18.
Simba inafanikiwa kutinga hatua hiyo ikiwa nafasi ya pili na kujizolea pointi tisa huku Raja Casablanca akiwa katika nafasi ya kwanza akiwa na pointi 13.
Wanaweka historia yakuingia kwenye nafasi hiyo kwa mara ya nne.
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Clatous Chama (3) dakika ya 10, 36 kwa penalti na dakika ya 70, Jean Baleke akishinda magoli mawili Dakika ya 32 na 65, huku Sadio Kanoute akishinda magoli mawili dakika ya 54 na 87.
Kwa ushindi huo Wekundu hao wa Msimbazi wanafanikiwa kujizolea milioni 35 zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akinunua kila bao linalofungwa kwenye michuano hiyo ya kimataifa kwa milioni 5.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa ugenini dhidi ya Hoyora Simba walikubali kichapo cha bao 1-0.