Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (anaebonyeza kitufe) akishuhudia maji yakitoka kwa mara ya kwanza kwenye eneo la Tegeta A ikiwa ni matokeo ya kukamilika kwa utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji wa Makongo hadi Bagamoyo uliotekelezwa na DAWASA. Mradi utanufaisha wakazi 450,000 kutoka Makongo hadi Bagamoyo. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja na (wa pili kulia) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndugu Kiula Kingu.