Home BUSINESS BENKI YA DCB YAAHIDI HUDUMA BORA KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA...

BENKI YA DCB YAAHIDI HUDUMA BORA KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto (kushoto), wakiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo, katika hafla ambayo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikabidhi hundi za mikopo kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika mapato ya ndani ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji hilo. Vikundi 16 vyenye akaunti katika Benki ya DCB vilikabidhiwa hundi ya shs 790,990,000.  

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro (katikati), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki (kulia kwake), wakikabidhi mfano wa hundi ya shs 790,990,000  kwa wawakilishi wa vikundi 16 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kama mikopo kutoka katika mapato ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Vikundi hivyo vina akaunti katika Benki ya DCB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Isidori Msaki akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki (kulia) na Diwani kata ya Kitunda, Victor Vedasto, wakiangalia baadhi ya bidhaa za wajasiliamali wakati wakitembelea katika mabanda ya wawakilishi wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Isidori Msaki (wa pili kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa (kulia), wakiwa katika hafla hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.

Kikundi cha uhamasishaji kikitoa burudani katika hafla ambayo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikabidhi hundi za mikopo kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika mapato ya ndani ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji hilo. Vikundi 16 vyenye akaunti katika Benki ya DCB vilikabidhiwa hundi ya shs 790,990,000. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro (katikati), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki (kulia kwake) pamoja na viongozi wengine, wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo kutoka katika  vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu mara baada ya hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Ilala kutoka kikundi cha Ua Waridi wenye akaunti katika Benki ya DCB wakipiga picha na mfano wa hundi ya shs 790,990,000 ambayo imetolewa kwa vikundi 16 vya wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Previous articleSIMBA SC YAFIKISHA ALAMA 6, IKIICHAPA VIPERS 1-0 MICHUANO YA CAF
Next articleHIGH-LEVEL THEMATIC ROUNDTABLE: VICE PRESIDENT STATEMENT
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here