– Akabidhi Vifaa vya Usafi kwa Shule zote za Mkoa wa Dae es Salaam.
– Awaelekeza Maafisa Elimu kutoa waraka wa kuelekeza kila shule kufanya Usafi na kupanda Miti.
Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.
Ikiwa kesho Ni Jumamos ya mwisho wa Mwezi ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam umetenga siku hiyo kwaajili ya Usafi wa pamoja, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya Usafi kwenye maeneo yao.
RC Makalla ametoa wito huo wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Usafi kwa Shule zote za Mkoa huo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es salaam ambapo amesema kwa siku ya kesho zoezi la Usafi kimkoa litafanyika Wilaya ya Ubungo eneo la Manzese na Wilaya nyingine zitaratibu Usafi kwenye maeneo yao kuanzia ngazi ya Mtaa hadi kata.
Aidha RC Makalla ameelekeza Maafisa Elimu kuandika waraka wa kuelekeza kila Shule kufanya Usafi na kupanda Miti* ili Kupendezesha Mandahari ya Jiji.
Hata hivyo RC Makalla amesema Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es salaam Ni endelevu hivyo ametoa wito kwa Wananchi kuzingatia Usafi kwenye maeneo yao.