Home LOCAL DC ILALA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI KATIKA DALADALA NA ASKARI...

DC ILALA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI KATIKA DALADALA NA ASKARI JKT

Na: HERI  SHAABAN.

MKUU wa Wilaya ya Ilala  Ng ‘wilabuzu Ludigija  na Maafisa wa Mazingira  wanatarajia kuzindua Kampeni ya Usafi February mwaka huu na Askari wa Suma JKT kukamata daladala ambazo azijaweka vifaa vya kuifadhi takataka. 

Mkuu wa Wilaya Ludigija aliyasema hayo katika kampeni endelevu za usafi zilizozinduliwa kata ya Vingunguti Dar es Salam. 

“Naagiza kwa Watendaji Idara ya Usafi na Mazingira mwezi February mwaka huu tuzindue kampeni ya Usafi katika daladala ambazo awajaweka vifaa vya takataka zikamatwe na kuchukulia hatua kwa kutupa taka ovyo wakamatwe wapigwe faini “alisema Ludigija. 

Ludigija aliagiza Askari kukamata daladala zote zisizo na vifaa vya kuifadhia takataka  na kuzitoza faini .

Alisema kwa sasa Wilaya ya Ilala safi maeneo yote katikati ya Mji maafisa mazingira wameweka vifaa vya Takataka. 

Ludigija aliwataka wananchi wa Ilala kujenga tabia ya kuwa wasafi katika mazingira yao kila wakati kwani usafi ni afya.

Ludigija aliwataka Wakazi wa Vingunguti Jimbo la Segerea wawe mabalozi wa mazingira katika maeneo yao  ikiwemo kutoa Elimu ya usafi kila wakati 

Aliwataka maafisa Afya na Watendaji kusimamia usafi katika maeneo yao kila kata ikiwemo kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali ambayo yalitolewa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wake Afisa Mazingira Halmashauri ya jiji la Dar es Salam Rajabu Ngoda alisema halmashauri ya jiji kwa siku wanakusanya takataka tani 1100 wanasafirisha tani 600 kwenda dampo ya Pugu Kinyamwezi. 

Ngoda alisema Kampeni ya Usafi ni endelevu kila kata inazinduliwa mwisho wa mwezi ikiwemo kutoa Elimu kwa wananchi wote. 

Mwisho

Previous articleDCB KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI
Next articleBenki ya DCB kupitia mfuko wake wa kuisaidia jamii wa DCB FOUNDATION wasaidia kampeni ya usafi wa mazingira Temeke.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here