Home LOCAL SERIKALI, PLAN INTERNATIONAL KUSHIRIKIANA VITA DHIDI YA UKATILI

SERIKALI, PLAN INTERNATIONAL KUSHIRIKIANA VITA DHIDI YA UKATILI

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wadau wa Shirika la Plan International katika Ofisi yake eneo la Mji wa Serikali Mtumba.

Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International, Peter Mwakabwale akielezea namna Shirika lake linavyotekelza afua mbalimbali katika jamii wakati wa kikao kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Shirika la Plan International wa pili kushoto ni Niabu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International, Peter Mwakabwale


Na: WMJJWM-DODOMA.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imekubaliana kufanya kazi kwa pamoja na Shirika la Plan International katika kuihudumia Jamii na kusaidia kwenye kutokomeza ukatili, kuondokana na mimba za utotoni na kuwa na ustawi wa jamii.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wadau wa shirika hilo katika Ofisi yake eneo la Mji wa Serikali Mtumba, amesema hiyo ni hatua ya awali za kufungua milango ili wadau wenye nia njema ya kufanya kazi na Serikali waweze kuingia na kukubaliana, maeneo ambayo watafanya kazi.

Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana kuweka afua zitakazosaidia kupambana pamoja na mambo mengine kukomesha ukatili na kuondokana na mimba za utotoni.

“Kama mnavyofahamu hii ni Wizara mpya ambayo imempendeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kuianzisha, hii inatoa fursa kwetu kusimama imara na kuwabaini wadau tutakaofanya nao kazi kwa ushirikiano, hivyo Plan wamekuwa  sehemu ya mwanzo huu mpya ambao kwa uzoefu wao wa miaka 30, tunaimani watakuwa msaada katika kuweka afua zenye manufaa kwa taifa” alisema Dkt. Dorothy

  “Tukikutambua wewe ni mdau na pengeni unahusika na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto, inakuwa ni fursa ya kumuunganisha na wataalam wetu ngazi ya Vijiji na Mitaa ambapo huko wataalam wetu wa maendeleo wa jamii watakao shirikiana nao” amesema Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, amesema kama Serikali inataka kuwatambua  wadau hao na mchango wao, ili waweze kuondokana na ukatili wa watoto wa Mitaani na mambo mengine yanayo kwamisha ustawi wa jamii yetu.

“Tunachotaka ni kujua mdau yupo wapi na nini Mchango wake, kila mtu na mchango wake kwenye jamii uweze kusikika na kuonekana ambapo hii itasadia kuwapanga wadau na shughuli gani yakufanya tunapo wapokea” amesema Dkt. Chaula.

Dkt Chaula, ameyataka Mashirika kushirikiana na kuunganisha nguvu katika utatuzi wa matatizo kwenye jamii kwani miongoni mwa “Mashirika zaidi ya 11,900 yaliyosajiliwa ni mashirika takriban elfu sita yaliyowasilisha taarifa zake mpaka sasa na haijulikani kama yaliyosalia yapo kweli ama lah” Alilisisitiza Dkt. Chaula

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International, Peter Mwakabwale, amesema, shabaha yao nikuwaleta kwa pamoja wadau wengine na mashirika mengine na kuona ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na kujua nani yuko wapi na anafanya nini.

“Yapo mambo ambayo Serikali inaweza kuiga na kutekeleza, mathalani jambo ambalo Serikali imejielekeza kwa sasa ni utengenezaji wa Mifumo ya TEHAMA, ambayo itasadia kuweka kumbukumbu sahihi za ufatiliaji mambo ya ukatili kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya taifa” amesema Mwakabwale.

MWISHO

Previous articleGEITA YAHIMIZWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA.
Next articleSTAMICO YAZIDI KUPAA HATIMAYE MGODI WA CHINI (UNDERGROUND MINE) -KIWIRA UPO TAYARI KWA UZALISHAJI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here