Home LOCAL MVUA YASABABISHA KIFO CHA MTOTO MIAKA 5.

MVUA YASABABISHA KIFO CHA MTOTO MIAKA 5.

Mtoto wa Miaka 5 aliefahamika kwa jina la Maryciana Lucas mkazi wa kitongoji cha Kayenze ‘B’ kata ya Bukoli wilaya ya Geita mkoani Geita amefariki dunia na wengine watoto wawili miaka 02, 10 kujeruhiwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maafa kijijini hapo.

Tukio hilo limetokea tarehe 25.2.2023 majira ya saa kumi na moja jioni ambapo mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha na kusababisha kifo cha mtoto huyo na kuacha majeruhi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishina msaidizi wa polisi Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na majeruhi wawili ambao ni Abdallah Juma miaka 2 Silvester Mateso miaka 10 ambapo wote ni wakazi wa kijiji cha Bugogo.

Kamanda Safia amesema pamoja na mvua hiyo kusababisha kifo imeharibu nyumba 91 ambapo kijiji cha Bugogo ni nyumba 72, kijiji cha Ikina nyumba 14 na kijiji cha ntono nyumba 5 pamoja na uhalibifu wa mazao mbalimbali.

Previous articleWAFANYAKAZI WA BARRICK NORTH MARA WASHIRIKI MBIO ZA KILI MARATHON 2023
Next articleBOT YAWATAHADHARISHA WANANCHI WANAOKOPA KWENYE TAASISI ZISIZO SAJILIWA .
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here