Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akimsikiliza mratibu wa Tamasha hilo Bw. Emmanuel Mabupa wakati akifafanua jambo wawaandishi wa habari leo.
Kampuni ya Msama Promotion ambayo imeandaa tamasha kubwa la Pasaka imetaja baadhi ya Waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao wamethibitisha kuwepo katika tamasha hilo litakalofanyika April .9. 2023, katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari Februari 24.2023 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampumi hiyo Alex Msama amesema kwamba tamasha la awamu hii litakua la aina yake kwani waimbaji nguli wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki.
Mkurugenzi huyo pia amesema kwamba Tamasha hilo linaenda samabamba na sherehe za miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani baada ya mtangulizi wake Hayati Dkt Jonh Magufuli kufariki dunia.
“Siku ya Tamasha la Pasaka tutaliombea Taifa letu na Viongozi akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania na kuliletea Taifa letu Maendeleo,tumekuwa tukishuhudia majanga mbalimbali yanajitokeza kwa nchi zingine hivyo kupitia tamasha hili tutafanya maombi ya kulinusuru Taifa letu na majanga mbalimbali kama vile Vita,Ukame , Njaa na Mafuriko” amesema.
Msama amesema Kwamba Tayari Baadhi ya Waimbaji Nguli wa Nyimbo za Injili kutoka Hapa Nchini na Nje ya Nchi wamethibitisha kushiriki katika Tamasha hilo lianalotarajiwa kuwa na mambo mengi mbalimbali yatakayofanyika huku akiwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia na kuimba kwa pamoja kwa ajili ya kumsifu Mungu.
“Waimbaji waliothibitisha kushiriki Tamasha hili ni Tumaini Akilimari kutoka Kenya,Joshua Ngoma kutoka Rwanda,Upendo Nkone ,Ambwene Mwasongwe hawa nikutoka Tanzania,pamoja na Mwimbaji Masi Masilia kutoka nchini Kongo ambaye anakuja kwa mara ya kwanza hapa nchini hivyo Watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudia tamasha hili” amesema kwa bashasha kubwa.
Nkuongeza kuwa “bado tunaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine kutoka Mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini,Uingereza na Marekani ili washiriki katika Tamasha hili ,hivyo wale watakaokubali kushiriki tutaendelea kuwafahamisha Watanzania,lakini kuna baadhi ya kwaya zimekubali kushirikiana nasi ikiwemo Zabron Singers.