Home LOCAL CCM KATA YA ILALA YAADHIMISHA MIAKA 45YA CCM KWA KUKAGUA MIRADI

CCM KATA YA ILALA YAADHIMISHA MIAKA 45YA CCM KWA KUKAGUA MIRADI

 MmM

NA: HERI SHAABAN, ILALA.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ilala kimeadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani kwenye sekta ya elimu.

Ukaguzi huo ulifanywa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Kata ya Ilala ambapo walikagua ujenzi wa vyumba 17 vya madarasa katika Shule za Sekondari Mivinjeni na Msimbazi yaliyotokana na fedha za Uviko – 19.

Akizungumza wakati wa kukagua vyumba hivyo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ilala, Habibu Nasser, amezipongeza shule hizo kwa usimamizi mzuri wa fedha hizo.

“Tumekagua madarasa yaliyojengwa kwa fedha za Uviko – 19 kweli tumeona, tunawapongeza kwa usimamizi mzuri wa fedha na kujenga kwa ubora,” amesema Nasser.

Aidha amewataka wananchi kama kuna kero hazijafanyiwa kazi wasisite kuziwasilisha kwa viongozi wa chama ili ziweze kutatuliwa.

Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Saad Khimj ambaye pia ni Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, amesema madarasa hayo yatamaliza changamoto ya wanafunzi kurundikana darasani na kuboresha ufundishaji.

Amesema pia wametenga Sh milioni 45 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mivinjeni na kwamba kati ya fedha hizo Sh milioni 25 zitatoka halmashauri na Sh milioni 20 zitatolewa kupitia Mfuko wa Jimbo la Ilala.

Kuna changamoto ya upungufu wa viti na meza za walimu pamoja na madawati, tunawahakikishia baada ya muda watoto wote watakaa katika mazingira mazuri na changamoto zote zitakwisha,” amesema Khimj.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Mivinjeni, Imani Kundema, amesema walipokea Sh milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 ikiwemo chumba cha maabara na kwamba vyote vimekamilika na tayari vimeanza kutumika.

Kwa mujibu wa mkuu huyo ujenzi wa vyumba hivyo umeongeza idadi ya wanaunzi wa kidato cha kwanza ambapo mpaka sasa tayari wamepokea wanafunzi 235 kati ya 328 waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi, Pantaleo Maghali, amesema walipokea Sh milioni 140 za ujenzi wa vyumba saba na kwamba tayari vimekamilika na kuanza kutumika.

Mwisho.

Previous articleKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIPONGEZA SIDO KWA KUENDESHA MFUKO (NEF) KWA MAFANIKIO
Next articleBENKI YA EXIM, MASTERCARD ZAINGIA MAKUBALIANO KUBORESHA MALIPO YA KIDIJITALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here