KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Limited, ambao ni waanzilishi wa kinywaji cha Konyagi, leo inazindua aina mbili mpya za Konyagi ikiwa ni mwendelezo wa chapa hiyo zinazoitwa Konyagi Fusion. Konyagi Fusion zimekuja katika ladha mbili tofauti ikiwemo Konyagi Fusion ya ladha ya Tangawizi & Limao na Konyagi Fusion yenye Ladha ya Nazi. Uzinduzi ulianza katika ubao wa matangazo ambao ulikuwa n bomba la kutoa vinywaji hivyo kwa bure kabisa katika maeneo ya Coco Beach. Konyagi tayari imeshajulikana kwani ilianzishwa zaidi ya miaka 40 iliyopita na imekuwa moja ya kinywaji pendwa kwa wengi.
Meneja wa Chapa ya Konyagi Fusion, Pamela Kikuli, anasema: āTunayo furaha kutangaza kuwa leo tunazindua kinywaji kipya cha Konyagi. Kama mnavyojua Konyagi imekuwa na historia kubwa tangu ilipoanzishwa miaka ya 1968. Kwa sasa tumeleta Konyagi zenye ladha mbili tofauti kwa ajili ya vijana wa kisasa ambazo ni Konyagi ya Tangawizi na Limao, na nyingine ina ladha ya Nazi.
Aliongeza: āTunataka wateja wetu wapate ladha tofauti na waliyoizoea. Konyagi Fusion ina asilimia 20% ya kilevi na kupatikana katika ujazo wa mililita 250.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, Timea Chogo, anaongeza āWakati Tunafanya Uchunguzi, tuligundua kuwa mojawapo ya mitindo ya kimataifa ya vinywaji vya spirit ni kutumia ladha mbalimbali katika pombe kali. Na hivyo tukaamua kutumia kinywaji chetu cha kizalendo kutengeneza Kinywaji kipya kinachofuata mitindo ya Kimataifa. Konyagi Fusion zinatumia Ladha za kusisimua na pia kuburushisha zinazjulikana kama Konyagi Fusion, Ginger and Lemon and Konyagi Fusion, Coconut. Tuna imani kubwa wateja wetu watazipenda Ladha hizi mpyaā.
Konyagi Fusion rasmi itazinduliwa Februari 17, 2023 katika Ukumbi wa Tipsy Coco, Dar es Salaam. Tunatarajia wateja wetu watapata fursa ya kuburika zaidi kwani kwa mara ya kwanza zitaanza kupatikana chupa za milimita 250 kwa sh. 5,000 na zitakuwa zinapatikana katika maeneo yote Tanzania.