Home BUSINESS BUCKREEF YATOA MSAADA WA MAGODORO YENYE THAMANI YA MILIONI 12 KATIKA GEREZA...

BUCKREEF YATOA MSAADA WA MAGODORO YENYE THAMANI YA MILIONI 12 KATIKA GEREZA LA WILAYA YA GEITA.

Na:  Costantine James, Geita.

Mgodi wa Buckreef umetoa  magodoro yenye thamani ya million 12 katika Gereza la wilaya ya Geita  mkoani Geita kwa lengo  la kuendeleza ushirikiano wa mgodi huo na jamii inayoizungkuka pamoja na kusaidia jamii katika mambo mbali mbali. 

Alisema hayo afisa rasilimali watu wa Mgodi wa Buckreef Bi. Domitila Damas ambapo alibainisha kuwa  mgodi wa Buckreef umetoa magodoro hayo yapayo 150 kwa lengo la kuongeza idadi ya magodoro kwenye gereza hilo ili kuwasaidia wafungwa mbali mbali waliopo katika Gereza hilo waweze kupata sehemu nzuri ya maradhi

“Kwanza kwa wito wa barua kutoka kwa mkuu wa mkoa kuweza kusaidia gereza letu hapa la wilaya ya Geita kwa ajili ya wafungwa ambao wapo kuongeza idadi ya magodoro ili waweze kupata sehemu nzuri ya maradhi ikizingati nisiku nzuri leo ya upendo basi tuko hapa kujumuika pamoja na serikali kuonesha upendo kutoka Buckreef” Alisema Bi. Domitila Damas Afisa rasilimali watu wa Mgodi wa Buckreef.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Wilson Shimo alitumia nafasi hiyo kuwataka Mkuu wa gereza hilo pamoja na wafungwa na mahabusu katika  Gereza hilo kutumia vyema magodoro  hayo waliopewa na wahisani   huku akiupongeza mgodi wa Buckreef kwa kutoa msaada huo na kuzita taasisi nyingine ziige mfano kutoka kwa Buckreefu kuchagia magodoro kwani Gereza hilo bado linauhitaji wa magodoro mia moja (100).

”Tumepokea godoro zipatazo 150 ambazo zitaenda kuongeza angalau na kuboresha hali ya maradhi kwa watu wetu ambao wako hapa gerezani lakini pia tuendelee kuwa omba mkuu wetu wa gereza wafungwa na mahabusu basi kuendelea kutumia vyema hiki ambao tumekipata kwa wahisani mbali mbali niwapongeze mno wahisani wote wakiwemo hawa wa Buckreef na hata makanisa ambayo hapo awali na yenyewe yalituchangia magodoro tukiomba pia hata kwa wahitaji wengine baadhi ya wahisani ambao wako tayari kuja kutusaidia kuchangia magodoro haya 100 yaliyo bakia basi yatakwenda kufanya angalau uwepo mzuri wa sehemu za kulala kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wetu” Alisema  Wilson Shimo mkuu wa wilaya ya Geita.

Kwa upande wake SSP Jovin Byala Bujwina Mkuu wa gereza la wilaya ya Geita kwa niaba ya watumishi wafungwa na magereza alisema magodoro hayo yataongeza idadi ya magodoro yaliyopu huku akisema bado hayajitoshelezi huku akiwaomba wadau mbali mbalali kulisaidia Gereza hilo katika mambo mbali mbali ikiwemo magodoro.

“Magodoro haya yataongeza idadi ya magodoro yaliyopo lakini bado hayajatosheleza kwa sababu lokapu bado ni kubwa sana nawaomba wadau wengine wajitokeze waweze kutuchangia magodoro ili watu ambao wapo ndani wasijione kama wametengwa na wenyewe ni sehemu ya jamii japo wako huku kwa matatizo ambayo wameshikiliwa na serikali kwa mda  baadhi yao wanaingia na kutoka kutokana na shughuli zinazofanyika katika halmashauri za Geita wahalifu wanaonekana kuongezeka kila kukuicha kwahiyo rai yangu kwa wadau wengine waweze kutusaidia kwa misada mingine.Alisema   SSP Jovin Byala Bujwina Mkuu wa gereza la wilaya ya Geita.

Previous articleRC GEITA AAGIZA KUMALIZIKA OPERESHENI YA ANWANI YA MAKAZI IFIKAPO APRILI 15, 2022
Next articleDCEA YABAINI MCHEZO MCHAFU WA WATANZANIA WALIOTUMIA MWANYA WA UVIKO 19 KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here