Na: Costantine James, Geita.
Wafanya biashsara Mbalimbali Mkoani Geita wameipongeza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita kwa kuwapa elimu juu ya mfumo mpya wa uwasilishaji ritani za kodi kwa njia ya kielektroniki hali itakayo wawezesha kuwasilisha ritani za kodi bila kufika ofisini.
Wafanyabiashara hao wamesema mfumo mpya wa uwasilishaji wa ritani kwa njia ya kielektroniki unawasaidia kupunguza mda kwa kupanga foleni katika ofisi za TRA na badala yake wanafanya wakiwa ofisini kwao.
Wamesema mafunzo hayo yaliyotolewa yamekuwa mhimu sana kwao kwani mfumo huo unawawesha kupata mkusanyiko wa mahitaji yao sehemu moja hali inayopelekea kurahisha utendaji kazi kwao.
Wameipongeza TRA kwa kuwaondolea changamoto mbalimbali zilizokua zinawafanya kwenda katika ofisi za Mamlaka hiyo kwa ajiri ya kutatuliwa na sasa taarifa zote wanazipata mtandaoni kiurahisi zaidi.
Ofisa wa huduma na elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita Jastine Katiti amesema mafunzo hayo waliyoyatoa kwa wafanya biashara ni kuhusu maboresho ya mfumo wa utumaji wa ritani za kodi lengo ni kuwapa uelewa juu ya mabadiliko ya mfumo huo.
Katiti amesema kupitia mafunzo hayo wafanya biashara pamoja na walipa kodi wameweza kuwaelimisha juu ya mabadiliko katika utumaji wa ritani za kodi TRA.
Amese maboresho hayo ya mfumo yatasaidia wafanya biashara kuokoa mda kwani mfumo huo sasa umeboreshwa na kuwawezesha kuingiza taarifa zao kwa haraka na urahisi zaidi.
Amesema mabadiliko ya mifumo mara nyingi yanaleta uwazi zaidi katika taarifa za kodi pamoja na taarifa zaidi juu ya maswala ya ulipaji wa kodi ndani ya Mamlaka hiyo.
Katiti amesema mwitikio kwa wafanya biashara juu ya matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki ni mzuri huku akiwataka wafanya biashara kujikita zaidi katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki inayotolewa na mamlaka hiyo.