Home LOCAL DCEA YATOA ELIMU, YATAKA TANZANIA HURU ISIYOKUWA NA MATUMIZI YA DAWA ZA...

DCEA YATOA ELIMU, YATAKA TANZANIA HURU ISIYOKUWA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akingungua mafunzo yaliyotolewa na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya yaliyofanyika mkoani humo.


Ni Kamishna Generali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) mada juu mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika mafunzo waliyoyatoa mkoani Arusha.

Katibu tawala Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia akifanya utambulisho katika mafunzo yaliyotolewa na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya yaliyofanyika mkoani Arusha.

Baadhi yawashiriki waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ndiye mwenyekiti wa kati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wakiwemo viongozi wa dini

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa ya kulevya imetoa elimu kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha, viongozi wa dini, madiwani na watendaji wa kata juu vita dhidi ya madawa hayo ili kwa pamoja waweze kushirikiana na kuhakikisha wanakuwa na Tanzania huru isiyokuwa na matumizi ya dawa ya kulevya.

Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Mkuu wa Arusha John Mongela alisema kuwa juhudi za serikali za kupambana na dawa za kulevya zinatakuwa ziungwe mkono na kila raia mzalendo kwani mzigo wa athari za dawa hizo unalifika taifa zima.

Mongela amewataka viongozi hao kuyachukua mafunzo hayo kwa umakini ili yakawe na manufaa katika kupambana na dawa za kulevya kwani serikali inatumia gharama kubwa kupambana na watu wanaotaka kuliharibu taifa lakini pia katika uwekezaji wa utoaji elimu hiyo.

“Baada ya mafunzo haya nendeni mkapige  vita matumizi ya dawa ya kulevya ili kuhakikisha vijana wanabaki na akili timamu kwa mustakabali wa taifa kwani madawa yanayosafirishwa yapo kwa kiwango kikubwa hivyo mkawe mabalozi,” Alisema Mongela.

Kwa upande wake Kamishna Generali wa mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya alisema kuwa wanachotaka ni kuhakikisha elimu inamfikia kila mtanzani ili waweze kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambapo hadi sasa watu wanaotibiwa kutokana na athari za dawa za kulevya ni 10,600.

“Tunachotaka ni taarifa juu ya watu wanasafirisha na kuuza madawa ya kulevya katika nchi yetu  na kuvunja mtandao huo ili tuweze kumaliza suala hili na kuwa na Tanzania huru isiyokuwa na matumizi ya dawa za kulevya,” Alisema Kamishna Generali Kusaya.

Alieleza kuwa  katika kipindi cha 2021 walikamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kilo 859.29 zilizoingizwa kutoka nchi za nje ambapo ni kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya kukamatwa tangu nchi kupata uhuru ambapo mafanikio hayo yalisababishwa na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yoa.

“Tukiendelea kupata ushirikiano mzuri tunaoupata kwa watanzania wote ni dhairi kwamba kila mmoja aliendelea kuchukia dawa za kulevya ni imani yangu hii vita tutaikamilisha ndani ya kipindi kifupi,”Alisema.

Alifafanua kuwa katika kipindi cha Januari 2021 Hadi hivi sasa  wamekamata kilo 950.8 za dawa za kulevya kutoka nje ya nchi lakini pia kuangamiza mashamba ya bangi zaidi ya hekari 10.5 na kukamatwa zaidi kilo 860 za mirungu ambapo watuhumiwa zaidi ya 500 wamekamatwa

Naye Askofu Stanley Hotae wa kanisa la Anglikana alisema kuwa ni vema serikali ikaingiza somo la vita dhidi ya dawa ya kulevya shule za msingi ili watoto ambao ndio vijana wa kesho wakue wakijua dawa za kulenywa nini na athari zake ni zipi kuliko kuja kuangaika kutoa elimu wakati wakiwa tayari wameshapata madhara.

Previous articleSIMBA QUEENS KUSHUKA DIMBANI KUIKABILI FOUNTAIN GATE LEO
Next articleMKUU WA MKOA WA RUVUMA BRIGEDIA JENERALI IBUGE AAGIZA TANROADS KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MADEREVA WASIOZINGATIA SHERIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here