Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.
UONGOZI wa timu ya Geita Fc umeweka wazi kuwa kwa sasa wamejipanga vyema kuelekea mchezo wao dhidi ya Coastal Union utaopigwa Katika Dimba la Nyankumbu Mkoani Geita.
Mchezo huo utachezwa Jumamosi inatarajiwa itakuwa ya kufa au kupona kwa timu zote mbili.
Kikosi cha Geita ambacho kipo katika nafasi ya 8 ikiwa micheza 14 huku ikiwa na alama 17 katika msimamo wa ligi,huku ikiwa imetinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Shirikisho la TFF maarufu kama Azam Federation.
Akizungumza na wanahabari Afisa habari wa kikosi hicho,Hemed Kivuyo amesema kuwa hali ya kikosi ipo imara na hakuna majeruhi hata mmoja katika kikosi.
Ameongeza kuwa mchezaji wao mmoja ambaye ni Streka yupo salama na amerejea katika kikosi ambaye alikuwa katika majukumu ya kifamilia.
Amesema kuwa mchezaji wao Kelvin Nashon amerejea katika kikosi huku kwasasa wanasubiri kufika katika muhafaka wa mazungumzo na klabu yao huko Afrika Kusini.
Amefafanua kuwa wanaendelea na mchakato wa kukamilisha mchakato wa ununuzi wa Gari la wagonjwa litakalotumika katika kituo cha afya kilichopo Halmashauri ya Geita mjini.
Ameongeza mpango wa manunuzi kwakufuata taratibu zote umeanza na mpaka kufika mwishoni kwa mwezi wa tatu Gari Hilo litakuwa tayari .
Pia fedha hizo zinatokana na mapato ya uwanjani pamoja na uuzwaji wa bidhaa zinazotokana timu hiyo pamoja na mapato ya ndani.
“Fedha zakununua Gari Hilo zimetokana na mapato ya Klabu pamoja na mapato kidogo ya ndani “Alisema Zahara.
Aliongeza kuwa kituo hicho Cha afya pia kimejengwa kwa mapato ya ndani lengo la kufanya hivyo ni kusaidia Halmashauri yao.
Hata hivyo timu hiyo leo imeingia makubaliona na wachezaji wa zamani kwa lengo la kuisadia timu na kutoa semina kwa wachezaji.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa wanasoka Veterans Nchini (UMSOTA), Paul Lusozi (Faza Lusozi) amesema kuwa amefurahishwa na maamuzi ya kikosi cha Geita kwa kuthamini thamani yao.