Home LOCAL LUDEWA YAZIDI KUNEEMEKA, WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA

LUDEWA YAZIDI KUNEEMEKA, WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA

Na. Damian Kunambi, Njombe
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Ludewa zimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha sh. Bl. 5.4 kwaajili ya kupunguza mlima kimelembe ambao umekuwa ni kikwazo kwa shughuli za usafirishaji na hasa madini ya makaa ya mawe.
Akisoma taarifa ya  mkakati wa ujenzi wa barabara ya Ludewa Manda Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Ruth Shaloah mbele ya kamati ya siasa Mkoa wa Njombe, kamati ya siasa wilaya ya Ludewa sambamba na viongozi wa serikali amesema kwa sasa tayari serikali imekwisha kutoa fedha kiasi cha sh.Bl. 5.4 zitakazo punguza mlima huo wenye umbali wa km. 4 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 10.3.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoani humo Deo Sanga amsema Rais Dkt. Samia Suluhu  amekuwa akitoa mabilioni ya fesha ili kuiletea nchi maendeleo ambapo kwa wilaya ya Ludewa imekuja miradi mingi ya maendeleo.
“Rais wetu kila kukicha anatuletea fedha Mabi na Mabii hihvyo tunakila sababu ya kumpongeza kwani juhudi zake za maendeleo zinaonekana kwa vitendo”. Amesema Sanga.
Hata hivyo kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kuondolewa kwa kikwazo hicho cha mlima kutakwenda kuokoa maisha ya watu kwani kuna watu wamepoteza maisha yao huku wengine wakipata ulemavu kutokana na ajali zilizokuwa zikijitokeza mahala hapo.
Naye mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema barabara hiyo ya Manda Ludewa ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Ludewa hivyo ameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha za kurahisisha mawasiliano hayo ya barabara.
”Barabara ni moja ya chanzo cha maendeleo na kukua kwa uchumi, hivyo endapo barabara hiyo itakamilika itarahisisha usafirishaji makaa ya mawe, biashara mbalimbali za mazao ya chakula kwakuwa kikwazo kinachozuia kupita magari makubwa kwa urahisi kitakuwa kimekwisha ondolewa”. Amesema Mwanziva.
Previous articleCHONGOLO AYATAKA MABARAZA YA MADIWANI NCHINI KUFANYA KAZI ZA KUJADILI MASLAHI YA WANANCHI
Next articleSERIKALI YAWABANA WANAOCHAFUA MAZINGIRA KWA KELELE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here