Wafanya biashara mkoani Geita wametakiwa kuachana na dhana ya matumizi ya risiti bandia badala yake wajikite katika matumizi ya risiti halali kwa leongo la kuchangia kodi serikalini itakayo saidia kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Hayo yamebainishwa na meneja msaidizi upande wa madeni na ulipaji kodi kwa hiari John Peter Njau wakati wa semina iliyofanywa na mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) mkoa wa Geita kwa wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani kutokana na mabadiliko ya mfumo wa ulipaji kodi.
Njau amesema kuna baadhi ya wafanya biashara mkoa wa Geita ambao wamekuwa wakitumia risiti bandia kwa lengo la kukwepa kulipa kodi kwa serikali hali ambayo anapelekea kwa mfanya biashara kupunguza kiwango pesa ambacho mfanya biashara alitakiwa kulipa hivyo amesema pale wanapo patikana wafanyabiashara wanaotumia risti bandia wao kama TRA wanawachukulia hatua kwa mjibu wa sheria za nchi.
“Risiti bandia ni risiti ambayo haitambuliki unapokuwa na risti bandia unapotosha mapato ya serikali unaweza ukadai madai ambayo sio sahihi kwahiyo unapunguza ile VAT ambayo ulipaswa kuilipa serikalini kwahiyo sisi tumeweka utaratibu kuwa kila mfanya biashara lazima katika manunuzi yake yote awe na risiti ambayo ina verification code (nambari ya uthibitishaji) kwa Geita tatizo la risiti bandia lipo tumewahi kukutana na baadhi ya risiti bandia na tumechukua hatua mbali mbali kwa mjibu wa taratibu na sheria” Amesema John Peter Njau meneja msaidizi ulipaji kodi kwa hiari.
Kwa upande wa wafanya baishara waliohudhulia semina hiyo wamesema mafunzo hayo waliyoyapata kutoka TRA yanamanufaa kwao kwani itawawezesha kutunza taarifa zao za kodi kwa urahisi hali itakayowasaidia katika kufanya tathimini ya kulipa kodi kwa serikali.
Wamesema elimu waliyo ipata kutokana na mabadiliko ya mfumo wa ulipaji kodi kutoka TRA itawasaidia kuokoa muda pamoja na kurahisisha kazi kutokana na kufanya kazi kwa njia ya mtandao.
“Leo tumepata mafunzo ya mfumo wa tathimini ya malipo ya kodi ya ongezeko la thamani kwetu sisi kama wafanya baishara kwanza inaokoa mda wa kuanza kukimbizana huku na kule lakini pia inarahisisha kazi kwa sababu tunapunguza matumizi ya vitu vingi kwa kufanya vitu kwa njia ya mtandao” Alisema Daniel Lakey mfanya biashara