.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibarahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdallah, Viongozi na Watumishi mbalimbali wa Mahakama pamoja na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakati akiongoza Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria yalioanzia katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Haki (IJC) na kumalizika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) leo tarehe 22 Januari 2023.
pamoja na eGA kuhakikisha kuwa Mahakama inapatiwa “Bandwidth” ya kutosha ili kuendesha shughuli zake kwa kutumia Tehama.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa wito kwa wananchi wanaohitaji kudai haki zao kuhakikisha wanafahamu kwanza haki hizo kwa kusoma na kutafuta elimu itakayowezesha kufahamu sheria na taratibu zinazoongoza haki inayotafutwa.
Amesema Wiki ya sheria itatumika katika kutoa elimu na kuwakumbusha wananchi namna ya kupata haki zao kwa njia sahihi na rahisi. Amesema wiki hiyo pia itatumika kuonesha namna mahakama inavyotumia teknolojia katika kufanya shughuli zake. Prof Juma ameongeza kwamba kwa matumizi ya Tehama, haki inayotolewa mahakamani itakua shidani na haki bora nabiliyowazi kwa wananchi na wale watakaofika mahakamani.
Wiki ya Sheria imeanza rasmi leo tarehe 22 Januari 2023 na inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Februari 2023