Na: Stella Kessy
KIKOSI cha simba kinatarajia kuwasiliana kesho baada ya kumaliza mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane uliopigwa Usiku wa Februari 27 mwaka huu.
Timu imeondoka mjini Oujda kuelekea Cansablanca ambapo mchana huu watapanda ndege hadi Dubai na kuunganishwa ndege hadi Dar es Salaaam ambapo itawasili uwanja wa ndege wa juliaus Nyerere majira ya saa saba na nusu mchana.
Hata hivyo meneja wa timu hiyo ya Simba Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri kiafya na hakuna majeruhi yoyote aliyepatikana katika mchezo dhdii RS Barkane.
“Tumeanza safari ya kurejea nyumbani na tunatarajia kufika kesho mchana, tunawashukuru wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna ambaye amepata majeruhi kwenye mchezo huu, na tukifika ni moja kwa moja kwenye maandalizi a mchezo wa ligi yataanza”amesema
Baada ya kuwasili kikosi kitaanza moja kwa moja maandalizi ya mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Biashara pamoja na Dodoma jiji kabla ya kushuka tena dimbani kurudiana na Barkane Machi 13 mwaka huu.