Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni na Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi, wakijadiliana jambo na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande, katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Katikati ni Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Sebastian Waryoba, akizungumza na Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Sebastian Waryoba, akipewa maelezo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi BoT, Bi. Consolata Shao, kuhusu Kurugenzi ya Utumishi na Uendeshaji alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Mkaguzi wa Mabenki Mwandamizi, Bw. Gwamaka Charles, akielezea jambo kuhusu namna BoT inasimamia sekta ya fedha nchini kwa mwananchi alietembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mfupi, Chuo cha BoT, Bi. Tulla Mwigune, akifafanua jambo kuhusu Chuo cha BoT kwa mwananchi alietembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo akitoa elimu kuhusu Alama za Usalama za Noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Afisa Sheria kutoka BoT, Bi. Happy Mlwale, akifafanua jambo kuhusu Dawati la Utatuzi wa Matatizo ya Wateja wa Huduma za Kibenki kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya. Kulia kwake ni Maafisa Sheria Bi. Catherine Manase na Bw. Ramadhani Myo.
Mchumi Mwandamizi BoT, Bw. John Mero, akifafanua jambo kuhusu Uchumi wa Tanzania kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya. Kushoto ni Meneja Idara ya Uchumi Tawi la BoT Mbeya, Dkt. Nicholaus Kessy na Mchumi Mwandamizi, Bi. Anjelina Mhoja (kulia).
Mchambuzi Mkuu wa Masuala ya Fedha BoT, Bw. Ephraim Madembwe, akitoa elimu kuhusu namna yakuwekeza katika Dhamana za Serikali za Muda Mrefu na Muda Mfupi kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala akifafanua jambo kuhusu namna Bodi hio inakinga amana za wateja wa mabenki nchini kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.