Home LOCAL BALILE: WADAU WANA SHAUKU KUONA MUSWADA SHERIA YA HABARI UKISOMWA BUNGENI

BALILE: WADAU WANA SHAUKU KUONA MUSWADA SHERIA YA HABARI UKISOMWA BUNGENI

Mwenyekiti wa Jukwaaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema macho na masikio ya wadau wa habari nchini, yanaelekezwa jijini Dodoma kusubiri muswada wa Sheri ya Habari ukisomwa kwa mara ya kwanza Januari hii.

Amesema kuwa mwezi huu jukwaa hilo linatarajia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itawasilisha Bungeni Muswada wa Huduma za Habari ili ujadiliwe na inshallah Mungu akipenda utapitishwa na kuwa Sheria.

Akizungumza leo tarehe 19 Januari 2023, katika Ofisiza TEF, Kisutu jijini Dar es Salaam Balile  ameeleza kwamba wana matumaini makubwa muswada huo utawasilishwa bungeni kama Waziri wa Habari,Mawailiano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye alivyoahidi mara kadhaa kuwa muswada huo utaingia bungeni na utajadiliwa.

“Ni matarajio yetu kwamba Mungu akipenda Februari mwaka huu utakuwa umepitishwa na kuwa sheria na baada ya hapo basi tuanze huo utaratibu mwingine wa kuunda vyombo vinavyotakiwa ikiwemo baraza huru la habari pamoma na kuangalia na utunzi wa kanuni zilitokana na mabadiliko mbalimbali.

“Kwa hiyo kimsingi tunaona kwamba muelekeo ni mzuri, maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa sasa na hamu yetu kubwa kuona kwamba muswada huo unaingia bungeni baada ya kuwa umeshindikana kwenye Bunge la Februari mwaka 2022, ukashindikana Septemba, ukashindikana Novemba,”amesema Balile

Ameongeza lakini safari hii wana imani kubwa kwasababu wameshazungumza na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari, wameshazungumza na watendaji wa Serikali.”Na ni matumaini yetu makubwa sana tunataraji tutauona muswada huo ukiingia bungeni na mambo yote yaweze kwenda vema.”

Previous articleBRELA YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU
Next articleRAIS SAMIA AKUTANA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA SYNGENTA CROP PROTECTION AG,DAVOS NCHINI USWIZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here