Home LOCAL ZUNGU AZITAKA HALMASHAURI KUANGALIA SUALA LA MATIBABU KWA WAZEE 

ZUNGU AZITAKA HALMASHAURI KUANGALIA SUALA LA MATIBABU KWA WAZEE 

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza na wazee wa Kata ya Kisutu Wilayani Ilala wakati wa kuzindua baraza la kata (kushoto)Mwenyekiti wa CCM Wilaya Said Sidde na Diwani wa Kisutu Khery Kessy. (Picha na Heri Shaaban).

Wazee wa Kata ya kisutu wakimsikiliza Mbunge wa Ilala Mussa Zungu.

 Na: Heri Shaaban (Ilala)

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amezitaka Halmashauri Nchini kuangalia suala matibabu ya Wazee waweze kupata huduma Bora za matibabu .

Naibu Spika Zungu aliyasema hayo akiwa Jimbo la Ilala kuzindua Baraza la Wazee Kata Kisutu .

Alisema huduma za matibabu ya Wazee katika vituo vya afya ni KERO amna kituo cha afya ambacho kinawapa kipaumbele wazee katika suala zima la matibabu nchini.

“Naomba Halmashauri kutazama upya suala la matibabu ya Wazee waweze kupata huduma Bora za afya wafikapo hospitali nashangazwa vituo vya afya wanashindwa kutambua Wazee wakati Hospitali zote Mali ya Serikali “alisema Zungu

Ameagiza utolewe waraka wa Serikali wa kutambua Wazee katika matibabu bila kupewa KERO wawapo kituo cha afya .

Mbunge Zungu alisema Sera ya Taifa Mabaraza ya Wazee yapo kisheria kila kata kwa ajili ya kusaidia serikali na inatambua umuhimu wao.

Mbunge Zungu alisema Wazee wanatakiwa kuunda mabaraza yao alafu kutoa ushauri katika kusaidia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Katika hatua nyingine Mbunge Zungu alisema kuna vijana wanagombana na Wazazi wao wanashindwa kuwa nao karibu wakati watoto wao wamesoma .

Aliagiza wazee washirikishwe katika miradi ya Serikali katika Utekelezaji wa Ilani na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mwaka jana alikutana na wazee wote kuzungumza nao na mwaka huu pia atakutana nao ni sehemu ya utaratibu wake kuzungumza na wazee

Akizungumzia Bima ya Afya iliyoboreshwa Mbunge Zungu alisema imewatambua wazee pamoja na makundi maalum wakiwemo walemavu.

Mwisho.

Previous articleHII HAPA SAFU MPYA YA KAMATI KUU NA SEKRETARIETI YA CCM 
Next article“HAKIKINI NAMBA KUEPUSHA UHALIFU” – NAIBU WAZIRI KUNDO 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here