Waziri wa maji Jumaa Aweso akitoa taarifa ya mafanikio ya wizara ya maji tangu serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani.
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa maji Jumaa Aweso amewataka wataalamu kwenda kusimamia miradi ya maji inayoendelea kote nchini katika kuhakikisha watanzania waishio mijini na vijijini wanapata maji safi na salama.
Aweso ametoa rai hiyo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya wizara ya maji ya mwaka mmoja tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya sita madarakani hafla iliyofanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa Rais Samia Suluhu ameonyesha waziwazi dhamira yake ya kumtua mwanamama ndio kicheani ambapo vijijini itatekelezwa miradi 1176 na mijini miradi 114 hivyo ni vema wataalamu wakasimamia vizuri na kuhakikisha miradi inatekelezwa ipasavyo.
Alisema kuwa Rais Samia amewaoa uelekeo wa wizara yao ya maji ambapo kila pembe ya Tanzania Kuna miradi ya maji inayoendelea kutekeleza kwani anatambua kuna rasilimali za maji toshelevu juu ya ardhi na chini ya ardhi ambapo juu ya ardhi kuna rasilimali za ujazo mita bilioni 105 na chini ya ardhi bilioni 20 ndio maana hataki kusiki wananchi wakiteseka kwaajili ya ukosefu wa maji.
“Anataka atuone wizara ya maji tukitekeleza miradi mikubwa na yakimkakati katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na kazi hii tumeshaifanya kwa vitendo na namwakikishi Rais kuwa miradi yote inayoendelea na tunayoenda kuianza nchi nzima tutaitekeleza kwa weledi na kuhakikisha watanzania waishio mijini na vijijini wanapata maji safi na salama,”Alisema Aweso.
Alifafanua kuwa katika kupambana na suala zima la uviko Rais Samia Suluhu amewapatia bilioni 139 ambazo wanakwenda kutekeleza miradi 218 katika ambapo katika kila Jimbo wanajenga mradi lakini pia kwenda kununua mitambo ya kuchimba visima 25 na kila mkoa utakuwa na kisima.
Aliendelea kusema kuwa nchi nzima kumekuwa na fursa mvua lakini imekuwa ikipotea baharini na kuleta maafa katika nchi ambapo Rais Samia anataka badala ya mvua kugeuka kuwa laana kwa kuleta maafa mvu hizi ziwe fursa kwa kilimo, uvuvi pamoja na wizara ya maji kutumia kupeleka maji safi na salama kwa wananchi hivyo kupitia fedha hizo wanaenda kununua seti tano kwaajili ya kuchimba jambo ambalo halijawahi kutokea.
“Kupitia fedha na sapoti ambazo ametupatia wizara ya maji upatikanji wa maji umeongezeka mijini na vijiji kwani tumetoka asilimia 70 ya upatikanaji wa maji na Sasa tuna asilimia 72.3 kabla ya 2025, asilimia 86 ya upatikanaji wa mji
na kwa miradi hii inayoendelea tutafikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini na 95 upatikanaji wa mijini kabla ya 2025,” alisema.
Alifafanua kuwa mwezi huu Rais Samia amewapatia Bilioni 41 kwaajili ya kulipa wakandarasi waliokuwa wakidai madeni yao ambapo wakandarasi wote wanaodai waende wizara ya maji machi 10 kwaajili ya kulipwa na hii ni kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao vizuri bila kukwamisha miradi.
Alieleza kuwa wanaelekea katika wiki ya maji ambapo Rais Samia Suluhu ameridhia kuwa mgeni rasmi na wizara hiyo imejipanga kuonyesha mafanikio kwa vitendo ya kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.