Home SPORTS SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 KWA MKAPA

SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 KWA MKAPA



Na: stella Kessy, DSM.

MABINGWA watetezi, Simba SC wameilaza Dodoma Jiji FC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 56 kwa penalti na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 74.

Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin inafikisha pointi 37, ingawa inabaki  nafasi ya pili, ikizidiwa pointi nane na jirani zao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 17.

Katika mechi zilizotangulia leo, Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wakati Coastal Union imewachapa wenyeji, KMC 2-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Hamisi kwa penalti dakika ya 22, William Kisingi dakika ya 82 na Rashid Chambo dakika ya 90 na ushei, wakati ya KMC yamefungwa na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 40 na Kenny Ally dakika ya 47.

Previous articleMAFUNZO YA UVIKO 19 KWA WADAU WA SEKTA YA UTALII YAZINDULIWA JIJINI MWANZA
Next articleKITENGO CHA WANAWAKE CWT ARUSHA WASHEREHEKEA WIKI YA WANAWAKE KWA KUWASAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here