Home LOCAL DC SHIMO AWATAKA WADAU WA MAENDELEO WILAYA YA GEITA KUSAIDI ZOEZI LA...

DC SHIMO AWATAKA WADAU WA MAENDELEO WILAYA YA GEITA KUSAIDI ZOEZI LA ANUANI ZA MAKAZI.


Na: Costantine James.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe, Wilson Shimo amewataka wafanya biashara  pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo ndani ya wilaya ya Geita kutoa ushirikiano kwa kuchangia nyenzo za anuani za makazi kwa lengo la kufanikisha zoezi hilo kwa wakati. 

Alisema hayo wakati alipokutana na  kuzungumza na wafanya biashara pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya wilaya ya Geita  ambapo aliwaomba wadau hao kujitoa ili kufanikisha zoezi hilo kwa haraka kwani linamanufaa makubwa kwa jamii na wananchi kwa ujumla.

Mhe. Shimo alisema kuwa wadau mbalimbali wa maendeleo wanayo nafasi kubwa ya kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii huku akiwataka wadau wenyewe kuchangia sehemu ambayo wanaweza ili zoezi hilo lifanikiwe kwa wakati.

“kwa yale ambayo mnafanya ni uzalendo wenu, ni utaifa wenu na kwamba mnafanya kwa manufaa ya jamii yenu nawaombeni muendelee kufanya hivyo lakini pia tuendelee kusaidia pale ambapo wenda tunaenda kusitahili kusaidia’’ 

“Zoezi hili ni msaada kwetu, sasa kama yoote hayo ni faida kwetu, nawaombeni mno, sasa na sisi tushirikiane pamoja, tushikane mikono,  pamoja kwa umoja wetu,” Alisema Mhe, Wilson Shimo.

Afisa Mipango  Halmashauri ya Mji wa Geita Barbara Mustafa wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo mjini Geita alisema kukamilisha zoezi hilo kuna uhitaji jumla ya Sh. 479,334,000/= kwa ajili ya kukamilisha zoezi la uwekaji anuani za makazi inayojumuisha namba za makazi na majina ya mitaa.

Alisema, pia kuna uhitaji wa mbawa za bati 236 zenye thamani ya Sh. 20,060,000, pamoja na mbawa za mbao 637 zenye thamani ya Sh. 54,145,000 sawa na gharama ya Sh. 85,000/= kwa kila mbawa nguzo  za anuani za makazi 2,102 zenye jumla ya gharama ya Sh. 315,300,000 sawa na thamani ya Sh. 150,000 kwa kila nguzo.

 Aidha mahitaji mengine ni vipande 70 vya nondo zenye thamani ya Sh 1,960,000/=, kokoto zenye thamani ya Sh.milioni sita, siment mifuko 90 kwa Sh 1,980,00 na gharama ya mafundi inayokadiriwa kufikia Sh. 79,889,000/=.

Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo wilayani Geita, Abdallah Msika alikiri anuani za makazi zina msaada mkubwa kwenye suala la ulinzi na usalama kwa jamii.

Hata hivyo Msika alitumia nafasi hiyo kuwataka wadau mbali mbali wenye uwezo wa kujitokeza kusaidia chochote kujitokeza  kwa wingi ili kuwezesha zoezi hilo kwani lina umuhimu mkubwa kwa jamii na litasaidia kurahisisha shughuli mbali mbali za kimaendelo ndani ya wilaya hiyo.
Previous articleBOHARI YA DAWA (MSD) IMETUMIA BILIONI 16.7 UJENZI KIWANDA CHA MIPIRA YA MIKONO (GLAVES) NA DAWA IDOFI MAKAMBAKO
Next articleMGODI WA NORTH MARA WACHANGIA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here