NA: HERI SHAABAN (ILALA).
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Saady Kimji amewataka Wana CCM wa Wilaya ya Ilala wafanye kazi kujenga Taifa waache kufanya kampeni ya kupanga safu ndani ya chama.
Saady Kimji aliyasema hayo kwa niaba ya Meya wa Halmashauri ya Jiji la DAR ES SALAAM Omary Kumbilamoto, ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kumuaga Afisa Mtendaji wa Kata ya Zingiziwa Tatu Nyamoga , ambaye ameamia Kata ya Ukonga na Mtendaji Ukonga ameamishwa Zingiziwa.
” Tunaelekea katika Uchaguzi wa chama chetu nawaomba ndugu zangu wana CCM wa Zingiziwa na Wilaya ya Ilala kwa ujumla tuwache makundi pamoja na kupanga safu tufanye kazi za chama Cha Mapinduzi sambamba na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kusimamia miradi ya maendeleo na kutekeza Ilani ya chama ” alisema Kimji.
Kimji alisema kanuni za chama zinazuia upangaji wa safu katika uongozi madhara yake makubwa watawekwa watu watakaoshindwa kukisaidia chama 2024 /2025 tukashindwa kusaka dola .
Alisema dhumuni la Chama Cha Mapinduzi CCM kushika dola hivyo wachague watu wenye mapenzi mema na Chama Chao watakaoweza kupeperusha Bendera ya chama hicho wakati wa chaguzi.
Akizungumzia Maendeleo ya Kata ya Zingiziwa Naibu Meya Kimji alimpongeza Diwani Maige Maganga kwa kuweka mahusiano vizuri baina ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi kushirikiana kufanya kazi .
Kimji alisema jambo alilofanya Diwani Maige ni jambo kubwa pia la kuigwa kwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwaaga Watendaji wa Kata kwa ajili ya mahusiano mazuri ya kazi katika kuisaidia Serikali Kata ya Zingiziwa.
Alisema Zingiziwa Kuna ujenzi wa kituo cha Afya kinajengwa pia ujenzi wa soko la kisasa amewataka Wananchi wa Zingiziwa waunge mkono juhudi za Diwani Maige za kuleta Maendeleo.
Aliwataka Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuweka mahusiano vizuri baina ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi Madiwani, Watendaji Kata kushirikiana na Chama katika Ili waweze kushiriki utekelezaji wa Ilani.
DIWANI MAIGE MAGANGA alisema anampongeza Afisa Mtendaji wake Tatu Nyamoga alimpa nguvu kubwa wakati wa kushika dola alimsaidia kwa asilimia 100 UCHAGUZI Mkuu wa Rais Wabunge na madiwani na kuakikisha CCM inashinda kwa kishindo na kuchukua dola.
Diwani Maige alisema lengo la hafla hiyo kujenga umoja na mshikamano Ili wengine waige mfano huo kuweka Serikali na Chama pamoja ili kusaka Maendeleo.
Akizungumzia Kata ya Zingiziwa alisema kwa sasa mafanikio makubwa yamepatikana sekta ya Elimu madarasa 12 yamekamilika ujenzi wa kituo Cha AFYA unaendelea na soko vyote vinafanywa na Serikali.
Akizungumzia Maendeleo mengine alisema mikakati yake mingine katika ujenzi wa Barabara Zingiziwa Omboza zinajengwa na TARURA amewataka Wananchi wake kumpa ushirikiano katika usimamizi wa miradi yote ya Serikali ambayo inatekelezwa.
Mwisho.