Watoto wawili Mmoja wa Miaka 3 na Mwingine mtoto wa mwaka mmoja na nusu wakazi wa eneo la Nyantorontoro B Halmashauri ya Mji Geita mkoani Geita wamefariki dunia kwa kutumbukia kisimani wakati wakicheza.
Mwakilishi wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita Emmanuel Ndoji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema watoto hao wametumbukia kwenye kisima hicho wakiwa wanacheza peke yao.
Amesema chanzo cha tukio hilo nikutokana na uzembe wa wazazi wao baada ya kuwaacha watoto hao peke yao hali iliyosababisha watoto hao kwenda kwenye bwawa hilo kuchota maji na kusababisha kifo chao.
Jeshi hilo limewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuacha kutelekeza watoto katika mazingira hatarishi hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.