Na: Lucas Raphael Sikonge ,Tabora
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu amewataka wataalam wanatoa huduma za afya kuboresha Mazingira ambayo yatakuwa ni rafiki kwa wagonjwa katika Vituo vya Afya ,Zahanati na hospitali ya wilaya ya Sikonge mkoani Hapa
Alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku mmoja aliyoifanya katika Wilayani Sikonge kwa kukagua maeneo ya Hospitali teule ya Wilaya ya Sikonge , Zahanati pamoja na ujenzi wa Jengo la Huduma za dharula (EMD) katika Hospitali ya Wilaya hiyo .
Alisema kwamba wataalam wanaotoa huduma za afya kwa kuahikisha wanaweka mazingara bora kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali zinazolewa kwa wananchi wilayani humo.
Hata hivyo alisema kwamba ameridhishwa na usimamizi mzuri wa Viongozi wanaosimamia Hospitali pamoja na Zahanati kwa kuboresha Mazingira ambayo ni rafiki kwa wagonjwa kupata huduma zuri za mamatibabu.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, alisisiza kuendelea kuboresha miundombinu ya Afya hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali ya awamu ya Sita inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya.
Makungu alisema kwamba kwa wilaya ya Sikonge ambapo ndio lango la kuingilia kwa kuwa ni njia inayopitia bandari ya Kalema Mkoani Katavi kuelekea Nchini Congo.
“Tutarajieni kupokea wageni wengi kutoka nchi za kusini kwa kuwa magari ya mizigo yatapita hapahapa Sikonge kuelekea bandari ya Kalema ambayo itakamilika mwezi wa Sita ambayo ndio inasafirisha bidhaa kwenda Congo.”
“pia watahitaji huduma mbalimbali zikiwemo za Afya,,,hivyo mjipange kuboresha zaidi miundombinu ya Afya kwa kuwa mtakuwa na wageni wengi zaidi kutoka nje” Msalika Makungu.
Kwa upande wake Mratibu kutoka Mfuko wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) Tausi Yunge aliwapongeza viongozi wa wilaya na wale wa Zahanati ya Sikonge ambayo ilipokea Tsh.Milioni 34.6 kutoka “RBF” kwa ajili ya ujenzi wa miondombinu kwa kuwa na Mazingira safi nje na ndani pamoja na mpangilio mzuri wa taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Naye,Mhasibu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simon Mality aliwasisitizia watumishi wa Afya kutumia mfumo wa kielektroniki wa kukusanya taarifa za wagonjwa pamoja kutunza kumbukumbu( GoT_HoMIs) kwa kuwa unarahisisha utoaji huduma kwa wagonjwa pamoja na kukusanya Mapato kwa Ufanisi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe ameahidi kutekeleza maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Katibu tawala.
Mwisho