Wakina Baba nchini wametakiwa kuacha tabia za kuwanyanyasa watoto wao wakuwazaa na kuwatelekeza kwa visingizio mbalimbali hali inayopekekea ongezeko la watoto waishio mitaa.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji cha Watoto wetu Tanzania, kilichopo Mbezi, Evans Tegeta wakati akipokea msaada wa mahitaji muhimu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuelekea sikukuu ya Mwaka mpya.
“Kina Baba wanawanyanyasa sana watoto wao wa kuwazaa, wakiume kwa wakike wanawachoma moto na kuwapa adhabu za kijeshi, wanawafukuza na kupelekea ongezeko la watoto wanaoishi mitaani, hii nsio changamoto kubwa inayopelekea watoto kuja hapa”
Aidha, akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo ukiwemo wa magodoro, vyakula na mavazi Afisa Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yamlihery Ndullah amesema NHC itaendelea kuwa sambamba na watoto wenye uhitaji katika kuhakikisha wanafikia ndoto zao.