Home LOCAL RIDHIWANI KIKWETE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO YA ARD

RIDHIWANI KIKWETE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO YA ARD

Na: Mwandishi Wetu.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali imejipanga kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka ya Wakulima na wafugaji.

Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo mapema Machi 15,2022 wakatj akishiriki uzinduzi wa Wiki ya Maji Simanjiro Mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Akitoa salamu za Wizara ya Ardhi, Mhe Ridhiwani Kikwete amempongeza na kumshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga bajeti itakayowezesha utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, mipaka baina ya Wilaya, Mikoa na Hifadhi na Usalama wa Ardhi.

“Wizara ya Ardhi imejipanga kuleta amani na utulivu kwa kutatua changamoto kwenye mipaka ya ardhi.” Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Mwisho.

Previous articleSOMA HABARI ZA MAGAZETI YA YALEO J.TANO MACHI 16-2022
Next articleKAMATI YA SIASA WILAYA YA MERU YAKAGUA MIRADI INAYOENDELEA KATIKA WILAYA HIYO YAAGIZA FUNDI KUONDOLEWA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here