Home LOCAL TMDA KANDA YA MASHARIKI YAKABIDHI MSAADA WA DAWA KATIKA HALMASHAURI YA MAFIA

TMDA KANDA YA MASHARIKI YAKABIDHI MSAADA WA DAWA KATIKA HALMASHAURI YA MAFIA

Na: Mwandishi Wetu, Mafia.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imekabidhi msaada wa dawa za binadamu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia zenye thamani ya zaidi ya milioni 6 kwa lengo la kusaidia matibabu ya wananchi wenye uwezo mdogo.

Dawa hizo zimekabidhiwa na Mkaguzi wa Dawa Bw Japhari Saidi kwa niaba ya Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki (Bw Adonis Bitegeko).

Akikabidhi dawa hizo mbele ya Kamati ya Dawa na Vifaa Tiba (CFDC) ya Halmashauri ya Mafia Bw Japhari ameeleza kuwa lengo la kukabidhi msaada huo wa dawa ni kusaidia wananchi wenye uwezo mdogo au wasio na uwezo kabisa kuchangia gharama za matibabu ili nao wapate dawa zenye ubora, usalama na ufanisi uliothibitishwa na TMDA.

“Dawa hizi zinatokana na sampuli zilizobaki baada ya uchunguzi wa kimaabara kukamilika na kufaulu vipimo.Hivyo, Ndugu Mkurugenzi naomba uzipokee ili ziweze kutumika kusaidia matibabu ya wananchi wa Mafia” Alisema Bw Japhari Saidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafia, Mwl Kassim Ndumbo ameishukru TMDA, kwa msaada huo na kuwaomba usiwe mwisho bali iwe na muendelezo kwa maslai ya Wananchi wa Wilaya ya Mafia.

Mwisho.

Previous articleMEENA : SERA YA HABARI 2003 ITAATHIRIWA
Next articleSERIKALI KUJA NA MWONGOZO WA KUCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here