Hayo yameelezwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya wenyeji Yanga na KMC ikiwa ni mchezo maalum wa kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Rais Mstaafu Kikwete amekuwa mgeni Maalum.
Rais Kikwete amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia sekta ya michezo imepata mafaniko makubwa hususani katika mchezo wa mpira wa miguu ikiwemo timu ya Taifa ya wanawake kupata ubingwa katika michuano ya kombe la COSAFA iliyofanyika Afrika kusini.
“Serikali imekuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza michezo na tayari imekamilisha mkakati wa Taifa wa uendelezaji wa michezo nchini, naamini kwa kupitia mkakati huu mtahakikisha mambo yanakuwa mazuri hasa katika upande wa timu ya taifa (Taifa Stars) ili tufurahi kwa kuiona timu yetu ikifanya vizuri .” amesema Rais Kikwete.
Aidha ameongeza kuwa amefurahishwa kuona mafanikio kwa wachezaji wa kike waliyoyapata kwa baadhi yao kuanza kwenda kufanya majaribio ulaya na kwamba hatua hiyo itaongeza ubora wa wachezaji hao na kuleta mafaniko zaidi kwenye timu ya Taifa ya wanawake.
“wachezaji wetu wanawake wameanza kununuliwa na timu za ulaya akiwemo Aisha Mataka aliyekwenda kucheza uko sweeden hii ialeta faraja kubwa katika soka la wanawake hapa nchini,
kwakweli Rais Samia ameupiga mwingi” ameongeza Rais kikwete.