Home BUSINESS ACK DAYOSISI YA MBEERE YAENDELEA KUFUNGUA MIRADI YA UCHUMI NA JAMII

ACK DAYOSISI YA MBEERE YAENDELEA KUFUNGUA MIRADI YA UCHUMI NA JAMII

Na: Maiko Luoga Kenya

Uongozi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mbeere nchini Kenya umeamua kuanzisha miradi ya maendeleo kwa lengo la kufanya uwekezaji na kujiimarisha kiuchumi ili kuweza kuendesha huduma ya injili kuhudumia jamii.

Disemba 19, 2022 Askofu wa Dayosisi ya Mbeere Dkt. Moses Masamba Nthukah aliongoza timu ya wataalamu wa Dayosisi hiyo kwenda katika eneo la Karuura Mutuovali kushuhudia makabidhiano ya shamba kubwa lililonunuliwa na Dayosisi ya Mbeere kutoka kwa mmiliki binafsi.

Askofu Masamba alisema Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 84 na rasilimali nyingi ikiwemo Shule ya kisasa, Hospitali, Matunda, Nyumba za watumishi na maji ya kutosha pamoja na miundombinu ya umeme.

“Tumekuja hapa Karuura Mutuovali kukabidhiwa rasmi shamba hili sisi tulilonunua kutoka kwa mwekezaji aliyeamua kutuuzia sisi Kanisa, tumeona vitu vingi vipo hapa nasi tumejipanga kuboresha na kuendeleza kwa faida ya Kanisa na jamii ya wananchi wa Mbeere na Kenya” alisema Askofu Masamba.

Bw. Joseph Njeru mfanyakazi katika shamba hilo akizungumza kwa niaba ya mwekezaji huyo, alisema wamekubaliana rasmi kuliuza shamba kwa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mbeere.

“Nikweli tumepokea wageni wa Ack Dayosisi ya Mbeere ambao wamekuja na aliyekuwa mmiliki wa shamba hili, tumefanya makabidhiano rasmi tunaamini Kanisa litaendeleza kazi njema iliyoanzishwa hapa” alisema Njeru.

Shamba hilo linapatikana umbali wa kilomita tatu kutoka mto Tana na katikati ya Bwa la kufua umeme la Kiambere na Kindaruma, pia lipo karibu na eneo maarufu lilalotoa mchanga wa kujengea majengo.

Baadhi ya Makasisi na waumini walioshiriki tukio hilo walipongeza jitihada za Askofu Moses Masamba za kuhakikisha anaibua miradi katika Dayosisi hiyo ambayo itasaidia kuhudumia jamii ya watu wa Kenya kiroho na kujiimarisha kiuchumi.

“Sisi mefurahi sana kuona maendeleo haya makubwa yanayofanywa na Baba Askofu katika Dayosisi yetu ya Mbeere Dkt, Masamba, licha ya kununua shamba hili lenye rasilimali nyingi pia ipo miradi mingine ya uchumi na maendeleo inaendelea katika Dayosisi yetu”

“Shamba hili lina fursa nyingi za biashara ambazo Kanisa litanufaika nazo, tumeona matunda mengi hapa ambayo tunaweza yatumia kuanzisha kiwanda cha juisi, pia maji yaliyopo hapa tunaweza kusindika na kuyauza kupitia kiwanda chetu kitakachoanzishwa hapa kwa mipango ya Bishop wetu” walieleza.

Rasmi sasa Shamba hilo linamilikiwa na Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mbeere lina ukubwa wa ekari 84, Shule kubwa ya msingi ya kuanzia Primary na junior Sekondari yenye huduma ya Bweni, Hospitali na vyanzo vikubwa vya maji ambavyo vitatumika kuzalisha maji kibiashara.

Pia yapo matenki makubwa ya maji, shughuli za kilimo cha umwagiliaji kibiashara, miti 1700 ya matunda aina ya maembe, mifumo ya umeme, maduka nane na nyumba 26 za kuishi wafanyakazi na chache kwaajili ya biashara.

Askofu wa Dkt, Moses Masamba alitoa wito kwa waumini wa Dayosisi ya Mbeere wanaoishi nje na ndani ya Dayosisi hiyo, Serikali, wadau na makampuni kuendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa maoni au ufadhiri wa fedha ili kuimaridha huduma ya injili na kusaidia wananchi.

Aliongeza kuwa Kamati ya uendeshaji itateuliwa na mamlaka husika ili kushirikiana na Wadhamini kusimamia na kuendesha shamba hilo liweze kutoa faida ndani ya Kanisa na jamii kwa ujumla.

Previous articleRUNWAY BAY YATIKISHA ZANZIBAR
Next articleTANROADS YATENGA BILIONI 17.8 MIRADI YA BARABARA DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here