Katikati ni Mhandisi Mbaraka Haruni Kutoka Shirika la Madini STAMICO makao makuu Dar es Salaam , Mhandisi Alfred Mhagama Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira kulia na Happy Mwakimage Kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira pia wakiwahuduamia wananchi mbalimbali waliotembelea Katika Banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Kilimo ya Nanenane Viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea kutangaza vyema faida za bidhaa yake ya mpya ya Mkaa Mbadala unaotokana na Makaa ya Mawe (Rafiki Briquettes)
Elimu hiyo imetolewa kwa wadau mbalimbali waliotembelea Banda la STAMICO katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Makangale mkoani Mbeya.
Wadau mbalimbali wamefurahishwa na Mkaa huo kwakuwa utakuwa ni suluhisho la ukataji miti hovyo na ni nishati mbadala kwa wananchi kuitumia badala ya mkaa au kuni
Katika Maonesho hayo wananchi mbalimbali waliweza kuona jinsi Mkaa huo unavyowaka na kwa muda mrefu bila kuzimika na kufurahishwa na ubora wake. Akiongea na wananchi hao Mhandisi Mbaraka Haruni aliwaeleza wananchi hao kuwa Mkaa huo kwa sasa upo kwenye hatua za majaribio na unaotengenezwa kwa kupitia mtambo wa Shirika uliosimikwa kwenye ofisi za Tirdo jijini Dar es Salaam.