Home LOCAL WAZIRI MKUU AAGIZA HOSPITALI YA KATAVI IANZE KUTOA HUDUMA

WAZIRI MKUU AAGIZA HOSPITALI YA KATAVI IANZE KUTOA HUDUMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Serafin ahakikishe ifikapo Januari Mosi , 2023 hospitali hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuu Kassim ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Disemba 12, 2022) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo inatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 12.4 itakapokamilika na imefikia asilimia 92 ya ujenzi.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi kuhakikisha ifikapo Disemba 23, 2022 awe amefikisha huduma ya umeme katika hospitali hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutawezesha kulaza wagonjwa 170 na hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia imeanza kuweka huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali zote za mikoa. “Kwa mara ya kwanza Katavi watapata huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali hii.”

Naye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

“Dhamira hii njema ya Rais Dkt. Samia tunaiona na ndio maana hapa manispaa ya Mpanda kunajengwa vituo vya afya vitano na vipo katika hatua ya umaliziaji, pia ametoa shilingi milioni 150 kwa ajili ujenzi wa zahanati”

Previous articleYETU MICROFINANCE BANK PLC KUWEKWA CHINI YA USIMAMIZI WA BENKI KUU YA TANZANIA
Next articleWATANZANIA TUTUNZE RASILIMALI ZA MISITU-MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here