Home LOCAL RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA KILIMO DODOMA

RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA KILIMO DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha Pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya Maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya ukaguzi wa mabanda mbalimbali ya wakulima pamoja na Wafanyabiashara leo tarehe 04 Aprili, 2022 Jijini Dodoma

Previous articleWANAFUNZI WA SHULE YA HEAVEN OF PEACE ACADEMY YA JIJINI DAR ES SALAAM WATEMBELEA JKCI KWA AJILI YA KUJIFUNZA MAGONJWA YA MOYO
Next articleNMB YAGEUKIA WAKULIMA, YAMWAGA MABILIONI KWA RIBA NAFUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here