Home BUSINESS DKT. NCHEMBA AWAOMBA WADAU WA SEKTA YA MIFUGO KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

DKT. NCHEMBA AWAOMBA WADAU WA SEKTA YA MIFUGO KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akizungumza jambo na baadhi ya Wadau wa Sekta ya Mifugo nchini, katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Jijini Dodoma, waliojadili namna ya kuboresha sekta hiyo kupitia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/2023. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Mb), Kulia ni Bw. Tixon Nzunda, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Wadau kutoka sekta ya uzalishaji wa maziwa na nyama nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Jijini Dodoma, akizunguza kuhusu nia ya Serikali ya kushirikiana nao katika kuboresha sekta hiyo kupitia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/2023.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya Wadau wa Sekta ya Mifugo nchini, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Jijini Dodoma, waliojadili namna ya kuboresha sekta hiyo kupitia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/2023. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Mb).

Baadhi ya Maafisa kutoka Serikalini, wakiongozwa na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Justine Japhet, wakifuatilia mjadala katika ya Mawaziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Mb) (hawapo Pichani), katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage wa Wizaraya Fedha, Jijini Dodoma.

Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka sekta ya uzalishaji  na usindikaji maziwa na nyama katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki (Mb), wa tatu kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Tixon Nzunda na kulia ni Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Justine Japhet. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) 

Benny Mwaipaja, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa rai kwa wadau wa sekta ya mifugo nchini kuisadia serikali kutimiza nia yake ya kuimarisha uzalishaji wa nyama na maziwa ili kuongeza tija na kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya watu.

Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo jijini Dodoma, alipokutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki, wataalam kutoka Wizara hiyo na Wizara ya Fedha na Mipango, pamoja na Wazalishaji binafsi katika sekta za maziwa na nyama nchini.

Dkt. Nchemba alisisitiza kuwa sekta ya mifugo itakuwa na mchango mkubwa katika kukuza kipato cha wananchi hususan vijana lakini pia itaongeza mapato ya nchi kwa kuzalisha bidhaa za nyama na maziwa zitakazo uzwa ndani na nje ya nchi hivyo kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.

Aliwataka wadau hao kuwa walimu wa kuwaongoza na kuwafundisha  vijana namna ya kuzalisha mifugo bora kwa ajili ya nyama na maziwa na kwa kuwa wana mtandao wa masoko, ni rahisi kwa wafugaji kupata maeneo ya kuuza mazao yao.

Dkt. Nchemba, alitoa wito pia kwa vijana na wawekezaji kuchangamkia fursa zinazopatikana katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili wajipatie ajira katika sekta hizo muhimu badala ya kuwaachia wazee peke yao kujihusisha na masuala ya kilimo na mifugo na kuahidi kuwa Serikali iko tayari kuwawezesha maeneo na mitaji.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki, aliwahakikishia wadau hao wanaomiliki kampuni na viwanda vya kusindika nyama na maziwa kwamba Serikali iko tayari kushirikiana nao kuboresha sekta ya mifugo ili ilete tija
Previous articleKONGAMANO LA KISAYANSI SEKTA YA MAJI LAFANA JIJINI DAR
Next articleGGML YATOA SH.MILIONI 50 KWA HOSPITALI YA CCBRT
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here