Home LOCAL SNV YANG’ARA KONGAMANO LA KISAYANSI NA UTAFITI KATIKA SEKTA YA MAJI...

SNV YANG’ARA KONGAMANO LA KISAYANSI NA UTAFITI KATIKA SEKTA YA MAJI JIJINI DAR

  Afisa miradi kutoka Shirika la maendeleo la uholanzi (SNV) Leyla Khalifa akionesha Tuzoa liyoshinda na Cheti alichokabidhiwa latika Kongamano la siku mbili la Kisayansi na utafiti katika Sekta ya maji lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere April 4,na 5, 2022 Jijini Dar es Salaam ambapo Leyla aliibuka mshindi wa Tuzo Maalum ya muwasilishaji bora na mtafiti mdogo (chini ya miaka 35) katika dhamira ya maji na usafi wa mazingira.


Afisa miradi kutoka Shirika la maendeleo la uholanzi (SNV) Leyla Khalifa (kushoto) akizungumza na wadau waliotembelea Banda la Shirika hilo katika Kongamano hilo April 5,2022, Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Mameneja Mamlaka za Maji Vijijini Erwin Singisa (wa pili kulia) akiwa na Meneja wa RUWASA Morogoro John Msengi (wa kwanza kulia) wakipata maelezo kuhusu mradi wa utunzaji mazingira kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga Angel Mwaipopo (wa pili kushoto) katika kongamano hilo.
 
Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Shirika la SNV Olivier Germain (katikati) akizungumza jambo na wadau katika Banda lao la maonesho Bara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akizungumza wakatia wa kufunga Kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili katika ukumbu wa kimataita wa mikutano wa Mwalimu julius nyerere April 5,2022 Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO.)
 
DAR ES SALAAM.

Shirika la maendeleo la uholanzi (SNV) lilikua moja ya mashirika makubwa kushiriki katika kongamano la maji la kisayansi kwa kupitia maonesho ya juhudi mbali mbali wanazozifanya katika sekta ya usafi wa mazingira kwa kupitia mradi wa WASH SDG. Kwa kushirikiana na wadau waliwasilisha mada mbali mbali pia ikiwemo matengenezo ya mkaa mbadala na urasimishaji wa kikundi cha wazibua vyoo cha WATU KAZI. 

Kwa kupitia mawasilisho haya, Afisa miradi kutoka Shirika la maendeleo la uholanzi (SNV) Leyla Khalifa ameibuka mshindi wa  Tuzo Maalum ya  muwasilishaji bora na mtafiti mdogo (chini ya miaka 35) katika dhamira ya maji na usafi wa mazingira. 
Tuzo hiyo imetolewa April 5,2022 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi  Nadhifa Kemikimba wakati wa kufunga Kongamano la siku mbili la Kisayansi na utafiti katika Sekta ya maji lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam lililowakutanisha wadau mbalimbali  wa Sekta ya maji na utunzaji mazingira.
Akizungumza na wadau hao mara baada ya utoaji wa Tuzo hizo Mhandisi Kemikimba amewapongeza wadau walioshinda Tuzo katika Kongamano hilo hususani vijana wenye umri mdogo kwa kazi kubwa wanayofanya katika jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.
Kwa upande wake Leyla Khalifa kutoka SNV amesema kuwa Shirika hilo lisilo la Kiserikali linatekeleza  mradi wa usafi wa mazingira mijini (WASH SDG) ambao unatekelezwa Arusha Mjini na Shinyanga Manispaa kwa kushirikiana na halmashauri za Manispaa na Jiji na Mamlaka za maji na kwamba mradi huo wa miaka mitano ulianza rasmi Mwaka 2017 na unatarajiwa kukamila mwaka huu. 

“Mradi wetu unalenga kuboresha maisha na afya za wanajamii kwa kuhamasisha tabia na huduma za usafi wa mazingira kwa kupitia jitihada mbali mbali ikiwemo kampeni ya usafi wa mazingira ya Mazingira Safi, Maisha Bora (msmbcampaign.com)” alisema Leyla.

Aidha katika maonesho hayo, Shirika hilo lilipata fursa ya wakuonesha bidhaa zao nyingine ikiwemo mkaa wa jambo moto unaozalishwa kwa kutokana na kinyesi cha Binaadamu na kwamba bidhaa hiyo inakaribibia kuingia sokoni hivi karibuni na kikundi cha wazibua vyoo cha watu kazi wanaopata ushirikiano kutoka kwa SNV na halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ili kurasimisha kazi zao.

Previous articleRAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MFUMO WA USAFIRISHAJI WA DHARURA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA M-MAMA JIJINI DODOMA
Next articleSPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA SPIKA WA UGANDA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here