Home BUSINESS TWIGA MINERALS CORPORATION YASHINDA TUZO YA KWANZA YA MLIPA KODI BORA NCHINI...

TWIGA MINERALS CORPORATION YASHINDA TUZO YA KWANZA YA MLIPA KODI BORA NCHINI TANZANIA

 

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari , Mheshimiwa Nape Nnauye, akikabidhi tuzo ya mlipa bora kwa Meneja wa Barrick nchini wa Fedha na Utawala ,Bw.Melkiory Ngido (katikati) katika hafla ya mlipa kodi ya TRA iliyofanyika jijini Dar es Salaam (Kulia) ni Meneja wa Kodi wa Twiga,Judith Chambua.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Habari Teknolojia ya habari Mheshimiwa Nape Nnauye na Watendaji Waandamizi wa TRA na Wizara ya Fedha katika picha ya pamoja na Watendaji kutoka taasisi mbalimbali zilizoshinda Tuzo ya mlipa kodi bora 2022.
 
Mgodi wa Twiga Minerals wa North Mara, umeshinda Tuzo ya mshindi wa kwanza ya Mlipa Bora katika hafla ya mwaka huu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kutoa tuzo kwa walipa kodi bora nchini.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana.
 
Twiga Minerals Corporation, inasimamia shughuli za: Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga; Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Tarime– pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi (Pangea) ambao pia upo Shinyanga na kwa sasa uko katika hali ya kufungwa.
 
Mnamo mwaka wa 2020, Twiga Minerals Corporation ililipa kodi ya mapato kiasi cha dola milioni $119, ambapo mwaka 2021, ililipa dola milioni $96.
 
Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliitambua Twiga, kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali kwa mwaka 2021. Kampuni yake tanzu – North Mara Gold Mine pia ilishinda tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa Wamiliki wa Leseni Maalumu za Uchimbaji katika Utekelezaji sera ya ushirikishwaji wazawa katika mnyororo wa uchumi wa madini (Local content) kwa mujibu wa Sheria ya Madini kifungu namba 123 mnamo mwaka 2021.
 
Akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha robo mwaka kwa vyombo vya habari mwezi Oktoba,mwaka huu, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation Dk, Mark Bristow, alisema kuwa Twiga imechangia kwa zaidi ya dola bilioni 2.187 katika uchumi tangu mwaka 2019. Kati ya hizo, dola milioni 878 zililipwa katika mfumo wa ushuru na kodi mbalimbali za serikali.
 
Kuhusiana na kusaidia ukuzaji wa biashara za ndani, Dk. Bristow alisema kuwa asilimia 80% ya manunuzi ya kampuni yenye thamani ya kiasi cha dola bilioni $ 1.025 yalikuwa ya bidhaa za ndani,
 
Previous articleMUHIMBILI KUANZISHA “SOBER HOUSE” NA KLINIKI YA MAGONJWA YA AKILI VIKURUTI 
Next articleMABALOZI WANAWAKE WAAHIDI KUIUNGA MKONO TAASISI YA ZMBF
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here