Home LOCAL WAUGUZI NA WAKUNGA TUMIENI LUGHA NZURI.

WAUGUZI NA WAKUNGA TUMIENI LUGHA NZURI.

Na: WAF – Shinyanga

Wauguzi na wakunga waaswa kuwa na lugha nzuri na ubunifu wa hali ya juu katika kuwahudumia wagonjwa Hospitalini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah katika kikao na wawakilishi wa wauguzi na wakunga kutoka katika wilaya za Msalala, Ushetu na Kahama Mkoani Shinyanga kujadili changamoto mbalimbali katika kada hiyo.

“Fanyeni kazi ya uuguzi na ukunga kwa moyo wote, kumekuwa hakuna kauli nzuri kwa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wetu wetu pindi wanapokuja katika Hospitali zetu” amesema Bi. Ziada.

“Wauguzi na wakunga wenzangu tubadilike, lugha kwa wagonjwa ikiwa nzuri kila mtu ata tamani kuja kutibiwa katika hospitali zetu “ Amesema Bi. Sellah

Ameendelea kusema Wauguzi na Wakunga wanahitaji kuwapa faraja wagonjwa na wateja wetu ili kuboresha huduma katika vituo vyao.

“Twendeni tukaboreshe huduma kwa kadri tulivyo fundishwa kwa kufuata kanuni taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya ikiwa ni kuwapa faraja wagonjwa wetu “ Amesema Bi. Sellah

Aidha Bi. Sellah amewasihi wauguzi na wakunga kuwa wabunifu katika kuwahudumia wagonjwa

“Unapokuwa mbunifu kwenye kumhudumia mgonjwa itasaidia kuongeza utoaji wa huduma bora katika vituo vyetu na kuwavutia wagonjwa wengi kuja Hospitalini” Amesema Bi. Sellah

MWISHO

Previous articleMKOA WA DAR ES SALAAM WAPOKEA VIFAA KINGA KUTOKA WATERAID TANZANIA KWA AJILI YA KUKABILIANA NA JANGA LA EBOLA
Next articleMAKTARI BINGWA WA MOYO WAENDELEA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here