Home LOCAL SERIKALI IMETENGA BILIONI 10.7 KUPAMBANA DHIDI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- DKT. MOLLEL

SERIKALI IMETENGA BILIONI 10.7 KUPAMBANA DHIDI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- DKT. MOLLEL

NAIBU Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo Novemba 2, 2022 amesema, Serikali imetenga shilingi Bilioni 10.7 kwa ajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza.

Dkt. Mollel amesema hayo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtoni Mhe. Idrissa Juma Abdul – Hafar katika kikao cha pili cha Bunge la 9, Jijini Dodoma.

Amesema, Mpango mkakati huo, umeainisha mikakati mahsusi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo, Kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta mtambuka, kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma.

Aliendelea kusema kuwa, mipango mingine ni pamoja na kuimarisha uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza, kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kujenga tabia ya kufanya mazoezi.

Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya afya kwa wote pindi Sheria hiyo itakapopitishwa na Bunge ili kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, hasa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan asmetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 149.77 kwaajili ya kuwapatia Bima wananchi wasio na uwezo.

Mwisho.

Previous articleRUWASA YAELEZA MIKAKATI YAKE HUDUMA YA MAJI VIJIJINI 
Next articleWAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here