Home INTERNATIONAL WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY

WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Massauni amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes ofisi kwake Dodoma, Januari 29, 2026 ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika Biashara ya Kaboni.

Mhe. Masauni amemshukuru Mhe. Tone kwa kuendeleza ushirikiano baina ya Norway na Tanzania huku akielezea namna ambavyo Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kinavyozidi kuimarika kadri siku zinavyokwenda.

Aidha Mhe. Masauni ameelezea mpango wa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu Biashara ya Kaboni kuanzia ngazi ya juu hadi kwa wananchi ili kuweza kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kuchangamkia fursa zinazopatikana.

Pia ameongeza namna Taifa linavyozidi kujidhatiti katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa moja ya njia katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira nchini.