Home ENTERTAINMENTS WAZIRI KOMBO ATEMBELEA MAONESHO YA 12 YA ZIFF ZANZIBAR

WAZIRI KOMBO ATEMBELEA MAONESHO YA 12 YA ZIFF ZANZIBAR

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ametembelea Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) 2026 yanayoendelea katika Kituo cha Maonesho cha Zanzibar, Dimani.

Maonesho hayo yalianza Disemba 29, 2025 yatamalizika Januari 16, 2026 ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Alipofika katika viwanja vya maonesho hayo Mhe. Waziri Kombo alitembelea pia Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar pamoja na wafanyakazi wa Wizara walioko katika ofisi hiyo

Maonesho hayo yanalenga kuangazia fursa za biashara na uwekezaji ndani na nje ya nchi.

Taasisi mbalimbali za serikali kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zinashiriki katika maonesho hayo na kutoa fursa ya kuelimisha umma juu ya huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zinatolewa na kuzalishwa na taasisi hizo.