

Wasanii nguli wa nyimbo za Injili kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuungana na waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa nchini kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka ambalo huandaliwa na kuratibiwa na Kampuni ya Msama Promotions ambapo kwa msimu huu linatarajiwa kufanyika kwa mikoa 20 likianzia na Mkoa wa Dar es Salaam.
Mapema akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amesema msimu huu wa pasaka Tamasha hilo litaanza tarehe 5 ya mwezi wa nne,likizunguka katika mikoa 20,kutoa burudani likiwa limesheheni wasanii mbalimbali wakubwa kutoka Tanzania na nje ya Tanzania lengo ikiwa ni kuwapa burudani waumini wa dini ya kikristo na wasio wa kristo sambamba na kutoa ujumbe wa kiroho.
Kadhalika Msama amesema wasanii wakubwa wanatarajiwa kupanda katika majukwaa hayo kutoa burudani kabambe kwa mikoa 20 kwani hiyo ni dhamira ya wao kama waandaji kuwapa burudani waumini wa Injili.
Ikumbukwe Tamasha hilo ambalo huandaliwa na Msama Promotions limekuwa maarufu kwa miaka mingi wakiwa ndio mabingwa wa kuleta wasanii wakubwa kutoka nchi balimbali za Afrika na Ulaya ambapo baadhi ya wasanii walowahi kutamba katika matamasha mbalimbali ya Pasaka ni pamoja na Mwimbaji bora kutoka Afrika Kusini .
Msama, katika kuongeza anabainisha kuwa msimu huu wasanii hao kutoka nje nao wataleta chachu ya Tamasha la Pasaka kama miaka iliopita ikiwa ni mwendelezo wa kuwa na waimbaji bora kama matamasha yaliuowahi kupita kwa kuwaleta waimbaji hao wengi .
Historia ya Tamasha la Pasaka inaendelea kupambwa na wasanii wengi maarufu ambapo kwa Mujibu wa Alex Msama amesema Tamasha hilo litakuwa la kishindo na lenye kutoa ujumbe wa kiroho.
Tamasha hilo la Pasaka hufanyika kila mwaka japo kwa miaka ya hivI karibuni lilisimama sasa limerejea kwa kishindo kwa mwaka huu.




