
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewasili katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Juu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam ya kukutana na kuzungumza na Mabalozi wa Mashina kwa lengo la kuimarisha uhai na mshikamano wa Chama.
Ziara hiyo inayofanyika chini ya kauli mbiu “ShinaLakoLinakuita” imelenga kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Tayari, Balozi Dkt. Migiro alianza ziara hiyo katika Wilaya za Temeke na Kigamboni, huku leo akiendelea na mikutano katika Wilaya za Kinondoni na Ubungo, kabla ya kuhitimisha ziara hiyo Januari 13, 2026, katika Wilaya ya Ilala.





