Home SPORTS RAIS SAMIA AWAKARIBISHA TAIFA STARS IKULU DAR ES SALAAM

RAIS SAMIA AWAKARIBISHA TAIFA STARS IKULU DAR ES SALAAM

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea tuzo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, iliyokabidhiwa kwake na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, ambaye kwa sasa ni Waziri Mteule wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), Profesa Palamagamba Kabudi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026. Rais Mhe. Dkt. Samia amekabidhiwa tuzo hiyo kutokana na kutambua mchango wa Serikali katika kukuza mchezo wa mpira wa miguu Barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya jezi ya Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ‘Taifa Stars’ iliyosainiwa na wachezaji kutoka kwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Bakari Nondo Mamnyeto, kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wanamichezo mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwapongeza mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, tarehe 10 Januari 2026. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Rais Mhe. Dkt. Samia aliwaandalia hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026. Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ilishiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ nchini Morocco na kufika hatua ya mtoano, ambayo ni historia kubwa kwa Tanzania tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.