Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha wadau wa Mahakama kilichofanyika tarehe 22 Januari, 2026 Jijini Dodoma.
Kikao hicho kilichoongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. George Masaju kililenga katika kujadiliana juu ya uboreshaji wa utoaji wa huduma za Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla





