Home SPORTS MISRI YAMFURUSHA BINGWA MTETEZI AFCON

MISRI YAMFURUSHA BINGWA MTETEZI AFCON

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Timu ya Taifa ya Misri, imefungashia virago mabingwa watetezi wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Ivory Coast kwa kuifurusha kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa usiku wa Januari 10, 2026 nchini Morocco.

Mchezo huo umepigwa ukikamilisha ratiba ya hatua ya robo fainali, na kutoa mwelekeo wa timu zitakazoumana Katika hatua ya nusu fainali.

Mchezo mwingine wa robo fainali, ulipigwa majira ya saa 1, za jioni kwa saa za Afrika Mashariki,  ambapo Nigeria imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuifunga Algeria mabao 2-0.

Kwa matokeo hayo, hatua ya nusu fainali kwanza Senegal watakutana na Misri, mchezo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizo mbili barani Afrika.

Nusu fainali ya pili Nigeria watachuana na na wenyeji wa michuano hiyo Morocco, michezo ambayo yote itachezwa siku ya jumatano ya tarehe 14/1/2025.